ENEO la Kariakoo, jijini Dar es Salaam, leo limerejea katika shamra zake nyingi za kawaida baada ya mvua zilizokuwa zikinyesha jijini kwa zaidi ya wiki moja kupungua.
Mtandao huu umezunguka mitaa mbalimbali ya Kariakoo na kukuta shughuli za biashara zikifanyika kwa kasi, hali iliyoelezwa kuwa kutokana na mvua kuendelea kunyesha wafanyabiashara walishuhudia mauzo ya biashara zao yakienda vibaya.
Hata hivyo, wateja ambao huishi na kununua mahitaji yao mbali na sehemu hiyo na ambao walionekana wakinunua bidhaa Kariakoo, walisema inapotokea hali ya hewa kuwa nzuri yaani kutonyesha mvua, hulazimimika kwenda maeneo ya Kariakoo ili kupata mahitaji muhimu zaidi.
(PICHA/STORI NA DENIS MTIMA/GPL)

Note: Only a member of this blog may post a comment.