Monday, March 2, 2015

Anonymous

MAKAVU LIVE: KOLETHA AWACHANA MASTAA WENZAKE WA KIKE KUHUSU MATUMIZI YA PESA WANAZOHONGWA!


Mayasa Mariwata/ijumaawikienda MSANII wa sinema za Kibongo, Coletha Raymond ‘Koletha’ amewataka mastaa wa kike kuzitumia vizuri fedha wanazohongwa na vigogo kwa kuwekeza kwenye miradi ili ziwanufaishe.
  Msanii wa sinema za Kibongo, Coletha Raymond ‘Koletha’.
Koletha alisema suala la wasanii wengi wa kike kuishi kwa kutegemea wanaume wakware lipo wazi kabisa, isipokuwa wengi wao wanajisahau kwa kuzitumia hovyo kwa starehe badala ya kuwekeza kwenye miradi. 

“Wasanii wengi wanategemea kuhongwa lakini wawe makini na hao wanaowahonga, kama ni gari wapewe kadi na chochote kile kiwe na uthibitisho ili mwisho wa siku wasiumbuke na kuchekwa lakini cha muhimu zaidi ni kuwekeza kwa maisha ya baadaye maana wengi wanaishia kujivunia nyumba za kifahari za kupanga wakati uwezo wa kujenga upo,” alisema Koletha.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.