Friday, March 20, 2015

Anonymous

Maamuzi ya Mwisho FIFA kuhusu fainali za kombe la dunia 2022 Qatar…


The World Cup
Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) limethibitisha tarehe ya kufanyika kwa fainali za michuano ya kimataifa ya Kombe la Dunia ambazo  zitakazofanyika nchini Qatar. 

FIFA imeweka hadharani tarehe ya fainali hizo wakati wa kikao chake jana huko Zurich, Switzerland ambapo itakuwa Desemba 18, 2022 huku ikisisitiza tarehe hiyo lakini Uingereza wameanza kulalamika wakidai ratiba hiyo mpya itavuruga ratiba ya ligi yao. 

Kawaida kombe la dunia hufanyika kati ya mwezi June na July lakini hali ya hewa ya Qatar imesababisha kubadilishwa kwa ratiba hiyo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.