Wednesday, March 11, 2015

Anonymous

LADY JAY DEE ATEMA CHECHE KUHUSU MIMBA!

Mwanamuziki nguli wa kike hapa Tanzania Lady JayDee ambaye kwa sasa anafanya poa na wimbo wake wa Forever amefunguka na kuonyesha kukerwa na kitendo cha baadhi ya mashabiki wake wa Instagram ambao walimuelewa vibaya baada ya kupost picha jana na kusema kuwa tumbo lake limevimba na kusema ana mimba.

"Imebidi nifute post Ili nielezee upya.Hivi watu hamuelewi kiswahili au ni nini ??? Nimesema tumbo limevimba sababu ya sahani,nikimaanisha mlo na nili post nakula hapo awali Sasa hayo maneno mengine yanatokea wapi? Au niwe naandika kichina? Kwani mliambiwa nitazaa Rais atakayewatoa katika shida zote mpaka mnishikilie mimba mimba..Hebu niacheni basi khaaa Nisiishi Kisa mimba? Aisee mnaboa sana. Basi niueni Kisa sijazaa Ili niwaondolee kero kabisa." aliandika Jide
Unalipi la kumwambia Jide hapo?! Tupia maoni yako hapo chini!

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.