Staa wa sinema na muziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi.
Gladness Mallya/Ijumaa wikiendaAlikuwa wapi? Baada ya kupotea kwa muda mrefu, staa wa sinema na muziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi hatimaye ameibuka na kueleza sababu za ukimya wake.
Katika intavyu hiyo, Snura alikanusha tetesi za kuzaa mtoto wa pili na kusisitiza ana mtoto mmoja na wanaosema maneno hayo wamekosa la kusema.Ijumaa Wikienda: Huoni kukaa kwako kimya mashabiki wamekusahau?Snura: Hawajanisahau kabisa na hilo nililithibitisha hivi karibuni kwenye shoo niliyofanya Msasani Club (Dar), ambapo walijaa tofauti na mwanzo japokuwa mwanzoni kabla ya shoo nilikuwa nawaza wamenisahau.
Snura: Unajua katika maisha yangu Hunter ndiye mwanaume wa kwanza kumuanika na sikuwahi kuanika mapenzi yangu kabisa kabla ya hapo. Sasa baada ya kuwa tunatupia picha mbalimbali kwenye mitandao watu walinifuata na kunieleza kwamba ninavyofanya siyo vizuri.
Nilichukua ushauri wao na kuufanyia kazi na mpenzi wangu nikamwambia, tukaacha tabia hiyo.
Hali hiyo ya kutokuweka picha ndiyo iliyozusha maneno kibao kwamba tumeachana lakini siyo kweli.
Ijumaa Wikienda: Hivi huoni kwamba Shilole amekufunika kwa sasa wakati wewe ulikuwa juu zaidi yake?
Snura: Hicho kitu hakipo na Shilole hawezi kunifunika kwani najua kwamba siku zote mbuyu hauwezi kugeuka mchicha.
HALI SI SHWARI HATA KIDOGO: MAMA WA MTOTO ALBINO ALIYEUAWA AMLIZA JB WA BONGO MUVI!
===>>SOMA ZAIDI HAPA!
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU
UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.
===>>SOMA ZAIDI HAPA!
ASANTE NA KARIBU
TENA!


Note: Only a member of this blog may post a comment.