Thursday, February 12, 2015

Anonymous

ALIKIBA AFUNGUKA KIHIVI KUHUSU KUFANYA KOLABO NA MASTAA WA AFRIKA!

Kuna time utakuwa unajiuliza maswali kuwa kuna umuhimu gani kwa wasanii wa hapa Tanzania kufanya kolabo na mastaa wa Afrika.
Sasa staa wa Bongo Fleva Ali Kiba amejibu swali lako na kusema;‘Katika kutangaza muziki inasaidia kiasi fulani lakini sio sana, muziki unaweza ukautangaza hata wewe mwenyewe, mimi binafsi muziki wangu nimeutangaza mbali sidhani kama Afrika hainijui bali inanifahamu sema tu kiukweli video zangu nilizokuwa nafanya hazikuwa katika quality nzuri huo ni ukweli naujua kwa hiyo sasa hivi tuko vizuri katika kujipanga nahakikisha kila kitu kitakuwa poa, hiyo inasaidia sana vile vile kubadilisha muziki na kuutangaza muziki wako katika msanii yoyote ambaye umemchukua labda wa Congo, Nigeria, Uganda, sehemu nyingine nyingi ili watu waweza kukusikiliza kwa urahisi na vile vile ni support kubwa inaonesha jinsi gani una ushirikiano na watu wengine‘-Alisema.
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.ASANTE NA KARIBU TENA

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.