Thursday, December 22, 2016

Unknown

Nimerudi Darasani Kujinoa Kimombo Ili Kujiandaa Kwenda Kimataifa -MC Pilipili Afunguka!

Mchekeshaji maarufu nchini, Emmanuel Mathias aka MC Pilipili amesema amerudi darasani kujinoa zaidi katika lugha ya Kiingereza, kama sehemu ya mikakati yake ya kwenda kimataifa.

Kwenye interview niliyofanya naye, Pilipili amesema japo Kiingereza ni lugha anayoielewa, angependa kuifanya iwe laini zaidi mdomoni mwake. Amesema tayari amemaliza kozi ya kwanza pale British Council na tayari ameshaona mabadiliko.
“Nimepiga pale miezi yangu mitatu, naanza mingine January halafu nitapiga module yangu ya tatu,” amesema.

“Nafanya hivyo kwa sababu naamini kwamba once the student is ready, teacher will appear. Kwamba nitakapokuwa tayari kwa ajili ya kimataifa, kwa hiyo hata gigs za kimataifa zitaanza kutokea kwa sababu unaanza kufanania.”

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.