KRC Genk ambao tayari walikuwa wanaongoza msimamo wa Kundi F kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa, wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0, magoli ya Genk yakifungwa na Jakub Brabec dakika ya 40 na Wilfred Ndindi dakika ya 83.
Nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta aliingia dakika ya 56 kuchukua nafasi ya nahodha wao Thomas Buffel, kwa sasa Mbwana Samatta anakuwa kaichezea Genk katika Europa League hatua ya Makundi kwa jumla ya dakika 126, mechi ya kwanza alicheza kwa dakika 77, ya pili 15 na 34.
Msimamo wa Kundi F iliyopo timu ya KRC Genk inayochezewa na mtanzania Samatta!

Matokeo ya mechi za Europa League
Note: Only a member of this blog may post a comment.