Najua watu wangu wanahamu ya kuona tuzo za MTV Mama 2016 zinazoandaliwa na kituo cha TV cha MTV Base Africa, lakini pia inawezekana kuna baadhi ya watu ambao wamebanwa na kazi na hawatapata nafasi ya kwenda Johannesburg kushuhudia tuzo hizo.
Diamond
Platnumz ni moja kati ya wasanii watakaopata nafasi ya kuperform katika
tuzo hizo, kama ulikuwa una mpango wa kukosa tuzo hizo hata kwa
kuangalia kwenye TV, Diamond ametumia ukurasa wake wa Instagram
kukujulisha kwa nini uhitaji kukosa tuzo hizo “Tafadhali
sana ndugu zangu naomba kesho msikose kutazama tunzo za MTVMAMA….
kijana wenu nimepanga kuwadhihilishia Ulimwengu Kuwa Africa Mashariki
kuna zaidi ya Wasanii”.
Note: Only a member of this blog may post a comment.