Monday, September 26, 2016

Unknown

Young Killer kufunga ndoa muda wowote!

Rapper Young Killer Msodoki amesema muda wowote kuanzia sasa atafunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Halimaty.
 Akiongea na Bongo5 Jumapili hii, Young Killer amesema kila kitu kipo tayari na siku yoyote atafunga ndoa.

“Kusema kweli sasa hivi tupo kwenye hatua za mwisho kabisa, yaani leo kesho mtasikia Young Killer amefunga ndoa,” alisema Young Killer. “Kwa sababu mambo muhimu yote yameshafanyika na kama vitabu vya mungu vinavyosema, mwanamke atamuacha baba yake na mama yake ataenda kwa mume wake,”

Rapper huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Mtafutaji’ amesema ana kila sababu ya kumuoa mpenzi wake huyo kwa kuwa ameishi naye kwa kipindi cha miaka 8.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.