Friday, September 23, 2016

Unknown

Rais Magufuli kafanya uteuzi mwingine leo September 23 2016

Kufuatia hatua ya Serikali kununua hisa zote za Bharti Airtel ambaye alikuwa mbia mwenza wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na hivyo Serikali kumiliki hisa za Kampuni hiyo kwa asilimia 100, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Waziri Waziri Kindamba kuwa Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL.

Waziri Waziri Kindamba ameteuliwa kushika nafasi hiyo kuanzia leo September 23 2016. Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura atapangiwa kazi nyingine.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.