Kuna uwezekano mkubwa video ya wimbo wa Forever wa Ruby isitoke tena. Muimbaji huyo ameitaja sababu ya kushindwa kuiachia kichupa cha wimbo huo.
“Video ya Forever sikuitoa kwa sababu niliona tayari nyimbo imesha-trend, not only that niliona mashabiki nilivyotoa lile shindano la kutafuta video queen na director walijitokeza watu wengi kwenye kuifanyia video,” amesema muimbaji huyo.
“So many ideas zilitokea kwahiyo nikaona ni kitu ambacho kimekubalika kwa mashabiki,” ameongeza.
Muimbaji huyo ameahidi kuachia ngoma kali na kufanya vizuri zaidi ya alivyowahi kufanya kwenye nyimbo zake alizowahi kuziachia.
Note: Only a member of this blog may post a comment.