Thursday, September 15, 2016

Unknown

Jose MOURINHO atoa sababu ya kumwacha Rooney katika safari ya Uholanzi

Nahodha wa klabu ya Manchester United Wayne Rooney hajajumuishwa katika kikosi kilichosafiri kwenda Uholanzi kwa ajili ya mechi ya Europa ligi dhidi ya Feyenoord.
Jose Mourinho akiongea na waandishi wa habari amesema haya kuhusu Wayne Rooney 

“Amecheza kila mechi tangu kuanza kwa msimu huu na amecheza dakika 90 katika timu ya Taifa ya England. Ninataka awe vizuri kwa ajili ya mechi zijazo . Anacheza katika eneo la ushambuliaji ambapo nina machaguo mengi.” Wachezaji 20 ambao wameenda Uholanzi ni De Gea, Romero, Johnstone, Darmian, Bailly, Blind, Mensah, Rojo, Smalling, Carrick, Fellain, Herrera, Mata, Memphis, Pogba, Schneiderlin, Young, Ibrahimovic, Rashford.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.