Aliyekuwa mgombea wa Urais kwa tiketi ya CHADEMA na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametembelea wakazi wa Kagera na kutoa pole kwa waathirika wa tetemeko la ardhi na kusema kuwa janga hilo si la kuiachia serikali pekee.
“Nawapeni pole, poleni sana, mwenzangu ameeleza kwa kirefu, sio mahali pa malumbano, lakini tunataka haki itendeke, tumekuja na msaada kidogo iko pale mkoani mtaipata, tuna hakika mtapewa misaada mingine kwa watanzania ambao wanajitolea na serikali inajitolea,” alisema.
Lowassa alisema madhara yaliyojitokeza ni makubwa hivyo watanzania wote wanabudi kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi.
Hivi karibuni Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Walemavu, Jenista Muhagama akiwa mkoani humo alisisitiza kuwa suala la tetemeko si la serikali peke yake bali ni la watanzania wote.


Note: Only a member of this blog may post a comment.