Friday, July 1, 2016

Unknown

SHILOLE Kiuno Anunua Mjengo Mpya Maeneo ya Chuo Kikuu Jijini Dar

Stori: Musa Mateja, Ijumaa
DAR ES SALAAM: Wakati baadhi ya watu wakiamini kukata viuno (nyonga) na kuimba muziki ni kazi fulani ya kawaida, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amewathibitishia kwamba inalipa baada ya kuvuta bonge la mjengo wenye thamani ya shilingi milioni 45.

Kwa mujibu wa chanzo, Shilole amevuta mjengo huo uliopo maeneo ya Gongo la Mboto, karibu na Chuo cha Kampala (KU) ambapo pamoja na fedha hizo alizonunulia, ameshateketeza jumla ya shilingi milioni 70 kutokana na ukarabati anaoendelea kuufanya.
“Ni nyumba f’lani hivi ambayo mwenyewe anataka kuibadili iwe katika mfumo wa kisasa hivyo kalazimika kuikarabati kwa kuboresha katika mfumo wa kisasa,” kilisema chanzo.

Alipotafutwa Shilole kuhusiana na ubuyu huo, alikiri kuwa kwa sasa ni mama mwenye nyumba baada ya kununua mjengo huo na anaendelea kuukarabati na kuainisha kuwa anategemea kutumia takriban shilingi milioni 100 hadi itakapo kamilika.

“Ni kweli kabisa hizo taarifa ulizopata zina ukweli maana nimenunua nyumba na hapa ipo kwenye hatua nzuri za ujenzi ambapo nimeanza kuikarabati na hadi naongea tayari kiasi cha milioni zisizopungua 70 zimeshateketea.

“Bado naendelea kujenga, kwani nataka iwe nyumba yangu ya mfano na hadi mwishoni mwa mwezi wa saba nitakuwa nimehamia, huku ikiwa imekamilika kila kitu.

“Nimeplani kuweka swimming pool ndani yake na garden za kutosha kwani ramani yangu tayari imefuatwa pamoja na kwamba nyumba nimeikuta imeshaanza kujengwa, ila naamini kabisa kwa juhudi zangu na mafundi wangu hasa ninavyowaona lazima mwisho wa mwezi wa saba nitakuwa nimeingia kwenye mjengo wangu, akili yangu yote ipo kwenye mjengo na hasa ukizingatia familia yangu yote inanisapoti ili nimalize,” alisema Shilole.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.