Sunday, July 3, 2016

Unknown

NAVY KENZO WASEMA KU-SHOOT VIDEO TANZANIA NI SAWA NA JIPU

Wasanii wanaounda kundi la Navy Kenzo, Aika Mareale (Aika) na Emmanuel Mkono (Nahreel) wameweka wazi kwamba ugumu wanaoupata wasanii wanapotaka kuchukua video za nyimbo ama filamu zao umekuwa na urasimu mkubwa, ndiyo maana hukimbilia nchini Afrika Kusini.Wasanii hao walisema hivi karibuni walijaribu kufanya moja ya wimbo wa msanii wao wanaotaraji kutoa kazi zake hivi karibuni lakini walifukuzwa na hata walipoomba vibali walishindwa kupata kwa wakati.

“Tanzania kuna tatizo kubwa la urasimu, msanii anapoomba vibali kwa ajili ya kushoot video ya wimbo wake, mfano juzi tu tulikuwa tunashoot video ya msanii wetu mmoja pale posta lakini tulifukuzwa tukalazimika kwenda sehemu nyingine za kukodi tukamalizia video yetu. Tanzania ni tatizo hata bendera ya taifa kupata ni tabu hadi tulipokwenda Afrika Kusini ndiyo tukapewa kila tulichotaka hadi bendera ya Tanzania ni ajabu sana ni sawa na jipu,” alieleza Nahreel.

Wasanii hao walitoa dukuduku hilo jana walipotembelea ofisi za Kampuni ya New Habari (2006) Ltd inayochapisha magazeti ya Mtanzania, Rai, Bingwa, Dimba na The African pamoja na kutambulisha lebo yao ya The Industryitakayokuwa ikimiliki wasanii watatu, Seline Rosalee na Wildad.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.