Ubuyu: Boniphace Ngumije na Hamida Hassan, Wikienda
DAR ES SALAAM: Kimenuka! Ndivyo
unavyoweza kusema kufuatia ubuyu ulioenea ‘town’ kuwa uchumba wa mastaa
wapenzi Bongo, Rammy Galis na Agness Gerald ‘Masogange’ unadaiwa
kuvunjika.
Ubuyu huo ulianza kutapakaa baada ya
picha ya Rammy ambaye ni mwigizaji wa Bongo Muvi na Masogange kuwekwa
kwenye kurasa mbalimbali za Mtandao wa Kijamii wa Instagram huku zikiwa
zimeambatana na maneno yanayodaiwa kuandikwa na jamaa huyo.
Maneno hayo yalisomeka: “Kwa nini mtu
husahau wema wote uliotenda? Utu wako wote unakosa thamani kwa kosa moja
ulilotenda, machozi humtoka mwanadamu pindi maumivu yakizidi moyoni.
“Unalia na kukesha kuomba msamaha lakini
mwenzio bado na ndiyo kwanza kamuweka mwanaume mwenzako kwenye WhatsApp
yake, sitakuja kusahau kwenye maisha yangu, nimeumizwa, leo nakubali.”
Picha hiyo ilipotupiwa mtandaoni, watu
mbalimbali walianza kushusha ‘komenti’ huku wengine wakimchana mshikaji
huyo kuwa u-handsome si kitu mjini bali mkwanja ndiyo kila kitu na kama
angekuwa vizuri, asingekimbiwa na mwanadada huyo.
WIKIENDA HALIKO NYUMA
Baada ya kuunyaka ubuyu huo, Wikienda halikuwa
nyuma, liliingia mzigoni na ‘kukontakti’ moja kwa moja na Rammy ili
kusikia yaliyomo yamo? Alipopatikana alisomewa kilichokuwa kinaendelea
mtandaoni ambapo alishikwa na kigugumizi huku akidai hataki
kulizungumzia jambo hilo hivyo liachwe kama linavyoonekana mitandaoni.
“Hili suala siwezi kabisa kulizungumzia,
ninyi liacheni hivyohivyo maana hata kama nimeachwa sidhani kama
inawahusu ni mambo binafsi na mimi ningependa tuongelee kazi kwa sasa
basi,” alisema Rammy.
RAMMY ABANWA
Mwanahabari wetu aliendelea kumbana Rammy ili kupata ‘floo’ yake ilivyokuwa kama ifuatavyo…
Wikienda: Rammy, pamoja na kuwa
umelizungumzia kwa kifupi, funguka ili mashabiki wako wajue
kinachoendelea kati yako na Masogange.
Rammy: Unajua sababu ya kutoongea haya
mambo ya Masogange ni kwa sababu nina mpenzi wangu ambaye tuko sawa,
nikiendelea kumpaisha huyo nampa kiki bure, huenda mambo
yakaniharibikia.
Rammy Galis na Agness Gerald ‘Masogange’
Wikienda: Hata hivyo, bado hujafunguka
vizuri kwani ishu ni nini kimetokea hadi mkazinguana, maana floo ya
ujumbe mtandaoni inaonesha wewe ndiye chanzo cha kumwagana kwenu?
Rammy: Nimeshakwambia haya mambo sipendi
kuyapa nafasi tena kama imeshatokea, imetokea, ukinihitaji nitafute kwa
masuala ya kazi tu!
MASOGANGE ASAKWA
Baada ya kumsikia Rammy, Wikienda lilimwendea
hewani Masogange ambaye ni video queen Bongo na kumsomea mashtaka yake
lakini alipopokea alisikiliza kisha akakata simu, alipopigiwa tena
hakupokea na hata alipotumiwa ujumbe mfupi hakujibu pamoja na kwamba
ulionesha umepokelewa kwake.
WALIKOTOKA
Uhusiano wa wawili hao una miezi kadhaa
tu ambapo kabla ya kuibuka kwa figisufigisu wamekuwa gumzo kwenye
mitandao ya kijamii kwani baadhi ya mashabiki wamekuwa wakiifurahia
‘kapo’ yao hivyo ubuyu wa kumwagana kwao utaibua mjadala mpya.
Note: Only a member of this blog may post a comment.