Friday, May 6, 2016

Anonymous

PETE YA UCHUMBA YA LULU YAZUA GUMZO... SIRI NZITO YAFICHUKA

Elizabeth Michael ‘Lulu’ akionyesha pete yake ya uchumba. MSANII maarufu wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameibua gumzo kubwa baada ya hivi karibuni kutinga kwenye Ukumbi wa Maisha Basement uliopo Kijitonyama jijini Dar akiwa ametinga pete ya uchumba. 

Lulu akiwa ametinga kigauni chake kifupi cheupe alifikia kwenye ‘red carpet’ na kuanza kupigwa mapicha huku akiweka mapozi tofauti lakini kila pozi alilokaa alihakikisha pete hiyo inaonekana. “Hee, huyu Lulu kavishwa lini hii pete, na nani? Au ndiyo yule bosi wa redio?” alisikika akihoji mmoja wa wadada waliokuwa eneo hilo na kuwafanya wengine waanze kumjadili. Ndani ya ukumbi huo ilikuwa vigumu kuongea naye na alipopigiwa simu ili azungumzie undani wa pete hiyo hakupokea

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.