Thursday, May 5, 2016

Anonymous

Majibu ya SNURA Baada ya CHURA Kufungiwa Yanafurahisha

Mchuma janga hula na nduguze lakini kwa Snura halitafuni janga lake na nduguze tu, bali mashabiki wake pia.
Baada ya wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo kuufungia wimbo wa Snura, Chura jana, muimbaji huyo anaonesha kutoshtushwa na hatua hiyo hasa kutokana na support anaiyopata kutoka kwa mashabiki wake.

Kwa ufupi haoneshi stress, walau kwa kile alichokiandika kwenye Instagram. “Ingekua ndio hela leo ningekua bilionea lo!!! Nawapenda sana kwakweli na nawatakia usiku mwema,” aliandika Snura kwenye Instagram.

Aliongeza hashtag: #utaipenda2_ndimuimekolea_malimao_kama__
210_habarizetuwanazo_ilazaohatuna.”
Pamoja na wimbo huo kufungiwa kuchezwa kwenye redio na TV, Snura aliagizwa kuhakikisha amefuta video zake zote mtandaoni.
-via bongo5

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.