Monday, May 9, 2016

Anonymous

DIAMOND Platinumz, Wizkid, Flavour Kutumbuiza Ukumbi Maarufu wa Barclays Center, New York, Marekani July 22

Ni ukumbi wa ndani kwa ndani maarufu mno jijini New York, Marekani nyumbani kwa wasanii wakubwa wakiwemo Jay Z, Beyonce, Justin Bieber, Rihanna, Drake, taja kila msanii mkubwa wa Marekani, amewahi kutumbuiza hapo.

Na sasa Diamond, Wizkid na Flavour, watakuwa wasanii wa kwanza wanaofanyia muziki Afrika kuwahi kutumbuiza kwenye ukumbi huo. Mastaa hao watatumbuiza kwenye tamasha la muziki la One Africa July 22, 2016 kwenye ukumbi huo wenye uwezo wa kujaza watu 20,000.

“We are about to Make a History America!!!…. Platnumz Diamond with my Fellow African brothers and Sisters will be Shutting the Barclays Center Down! On the 22nd Jully 2016 in New York!…. 20k Seat Capacity!…Now make sure you tell your Friend to tell a Friend,” ameandika Diamond.
Barclays Center ni ukumbi unaotumika kwa shughuli mbalimbali na upo Brooklyn, New York City. Pia hutumika kama uwanja wa nyumbani wa timu ya kikapu ya Brooklyn Nets pamoja na New York Islanders ya National Hockey League.
Show ya kwanza kufanyika kwenye ukumbi huo ilikuwa ya Jay Z, September 28, 2012.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.