Akizungumza katika kipindi cha Clouds TV Ijumaa hii, TID amesema hali hiyo ilimfanya atoke na wasichana wengi.
“Nilikuwa ‘namdate’ Wema Sepetu akaniambia sikutaaki, tangu kipindi
hicho nimekuwa na wasichana wengi. Ikitokea Wema anataka kurudi hakuna
nafasi, I’m occupied,” alisema TID.
TID amesema katika kipindi hicho aliumizwa sana na jinsi magazeti yalivyokuwa yanamuandika vibaya.
“Wakati huo mitandao ya kijamii haikuwepo lakini wamagazeti
walizichukua picha na kufanya yao, it was bad. Mimi nikasema sawa lakini
niliumia sana,” alisema TID.
Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Confidence’ aliyomshirikisha Joh Makini pamoja na Dully Sykes.
Note: Only a member of this blog may post a comment.