Saturday, April 9, 2016

Anonymous

Msanii Huyu Anataka Kumrithi ALI KIBA Kwa JOKATE KIDOTI


Picture (4) 
Mwanamuziki anayetamba na wimbo wake wa Nipe Wakaseme, Sitta Richard ‘Starick’.
Na Mayasa Mariwata
Mwanamuziki anayetamba na wimbo wake wa Nipe Wakaseme, Sitta Richard ‘Starick’ amesema yupo kwenye mchakato wa kuhakikisha anamrithi msanii Ali Salehe Kiba kwa mwanadada Jokate Mwegelo kwani ni binti aliyekuwa akimzimikia kinoma.

jokate12
Mwanadada Jokate Mwegelo.
Akipiga stori na Ijumaa, Starick alisema ni muda mrefu Jokate amekuwa akimkosesha usingizi lakini alikuwa akishindwa kumtokea kutokana na kwamba Kiba alikuwa amejimilikisha.
“Katika vitu ambavyo mwaka huu vimenifurahisha ni kusikia Jojo na Kiba wamefungiana vioo, nilikuwa namlia mingo tangu kitambo yule mdada, nampenda sana na sasa wakati wowote mnaweza kusikia lolote,” alisema.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.