Sunday, April 10, 2016

Anonymous

MAIMARTHA JESSE Aibuka na Malkia wa MSAMBWANDA!

Maimartha Jesse ‘Mai’ ambaye ni Mtangazaji wa Azam TV anasaka malkia wa kukata mauno ‘Msambwanda’ kupitia nyimbo za Taarab, Kisingeli na nyimbo za Mchiriku ambapo atakayeibuka mshindi atapozwa na zawadi ya bodoboda.

Mai aliitonya safu hii kuwa, ameamua kufanya shindano hilo kwa ajili ya kuinua vipaji na kuwapa ajira baadhi ya wasichana wanaokata nyonga.
“Si unanijua huwa napenda kuwainua wasichana wenzangu kupitia shoo mbalimbali! Mimi siko kama watu wengine, najivunia kuona mtu anaendesha gari kupitia mgongo wangu au kama hivi pikipiki itakuwa ni ajira kwa mtu,” alisema Maimartha.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.