Stori: Aplina Philipo, Wikienda
MBEYA: Mshtuko! Tofauti na utaratibu
uliozoeleka, maiti ya aliyekuwa sangoma maarufu, Mzee Kalinga (80),
mkazi wa Kijiji cha Chimala Muwale Wilaya ya Mbarali jijini hapa
aliyeaga dunia akiwa na wake 15, watoto 102, wajukuuu 216 na vitukuu 16,
imezikwa usiku ikiwa na masharti kibao.
Mwili wa Mzee Kalinga ukiingizwa kaburini.
Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki
iliyopita mara baada ya sangoma huyo ambaye enzi za uhai wake alikuwa ni
mganga wa kienyeji aliyetoa huduma ya kutibu maradhi kwa kutumia miti
shamba.
Akizungumza na Wikienda, mmoja wa watoto
wa marehemu, Shabani Kalinga alisema kuwa, baba yao alitoa maagizo kuwa
siku akifa azikwe ndani ya nyumba yake majira ya saa 4:00 au saa 5:00
usiku na maiti yake ifunikwe kwa ngozi ya mnyama atakayechinjwa na nyama
yake iliwe usiku.
Kalinga enzi za ujana wake.
Hata hivyo, Shabani, ndugu na jamaa
wengine wa marehemu walidai kwamba walishindwa kumuuliza enzi za uhai
wake ni kwa nini akifariki dunia azikwe kwa mtindo huo.
“Hata sisi tulipigwa na butwaa na
kuamini pengine masharti hayo yalitokana na aina ya kazi ya uganga
aliyokuwa akifanya,” alisema mmoja wa wanandugu hao.
Waaombolezaji wakiwa msibani
Mashuhuda wa mazishi hayo walishangazwa
na kitendo hicho cha sangoma huyo kuzikwa usiku kwani hawakuwahi
kushuhudia msiba wenye masharti kama hayo.
Ukiachilia mbali kuzikwa usiku, pia alizikwa ndani ya nyumba yake na kuacha gumzo kijijini hapo.
Note: Only a member of this blog may post a comment.