MAMBO vipi mpenzi
msomaji wa Mpaka Home? Spidi yetu ni ileile 120, tunakupa fursa ya
kuweza kujua maisha halisi ya mastaa mbalimbali wakiwa nyumbani.
Leo tunaye Video Queen, Lulu Abbas ‘Lulu
La Diva’ anayeishi maeneo ya Magomeni jijini Dar, twende pamoja kujua
mengi kutoka kwake:
…Akichoma ubani.
Mpaka Home: Mambo vipi, Lulu mimi nilijua ungeniambia unakaa Masaki kumbe unaishi Magomeni?
Lulu: Hahaa! Unajua siku zote mkataa kwao ni mtumwa. Mimi naishi hapa Magomeni bwana.
Mpaka Home: Kwa uelewa wako, unafikiri nyumba ya staa inatakiwa iweje?
Lulu:
Mimi ninafikiria inategemea na uwezo wa mtu kwa kweli lakini japokuwa
hata kama huna uwezo wa kukaa nyumba kubwa, unaweza kuitengeza ndani
ikaonekana tofauti.
Mpaka Home: Maisha yako ya kawaida yakoje hapa mtaani?
Lulu: Mimi ni mtu wa kawaida sana, ninachojisikia nafanya. Nikitaka kula muhogo kibandani nafanya hivyo sitaki maisha ya kujikweza.
Mpaka Home: Nimeshangaa sana kukukuta jikoni nilidhani mambo ya moto na wewe ni vitu mbalimbali!
Lulu: Nashukuru kwa
kuwa umenikuta mwenyewe maana usingeweza kukubali kama napika, lakini
mimi chakula ili nikisikie lazima nikipike mwenyewe kwa mkono wangu.
…Akiandaa chakula.
Mpaka Home: Vipi hapa unaishi na shemeji maana huku ndani si mchezo?
Lulu: (Haaah…haa)
naishi peke yangu lakini leo yupo mama yangu ni mgonjwa, bado sijaolewa,
nikipata mume nitaenda kuishi kwake siyo yeye aje hapa.
Mpaka Home: Nini hasa unachokipenda kwenye nyumba yako?
Lulu: Napenda sana usafi. Uchafu ni adui yangu ndiyo maana unaona hapa kila wakati nafukuzana na nzi.
Mpaka Home: Ukipata wageni ni kitu gani unapenda kuwaandalia ili kuwafurahisha?
Lulu: Pilau ndiyo chaguo la kwanza maana ni chakula kinachopendwa na watu wengi.
…Akitengeneza nywere
Mpaka Home: Kila mtu ana sehemu yake ambayo anaipenda nyumbani, kwako wewe ni wapi unapopapenda zaidi?
Lulu: Napenda sana kwenye kioo kila mara nikae nikijiangalia basi.
Mpaka Home: Hujawahi kufikiria kuwa na nyumba yako?
Lulu: Ndicho kitu
kinachoniumiza kila kukicha unajua ukipanga nyumba huwezi kuipamba
unavyotaka lakini najua nitafanikiwa maana najipanga kwa ajili ya hilo.
Mpaka Home: Nakushukuru sana Lulu kwa ushirikiano.
Lulu: Karibu tena.
Note: Only a member of this blog may post a comment.