Kama wewe ni mfuatiliaji wa mambo ya
filamu, jina la Gisela Joseph ‘Pinkieto’ litakuwa si geni kwako. Huyu
alikuwa ni sekretari wa marehemu Steven Kanumba lakini pia msanii
aliyeigiza kwenye filamu mbalimbali.
Wiki hii kupitia safu hii tunaye akijibu maswali 10 ambayo aliulizwa na Mwandishi Wetu Hamida Hassan. Unataka kujua ni maswali gani aliulizwa na akajibu vipi? Fuatilia mahojiano hapa chini… Ijumaa: Kifo cha Kanumba kimeathiri vipi maisha yako ya kisanii?
Wiki hii kupitia safu hii tunaye akijibu maswali 10 ambayo aliulizwa na Mwandishi Wetu Hamida Hassan. Unataka kujua ni maswali gani aliulizwa na akajibu vipi? Fuatilia mahojiano hapa chini… Ijumaa: Kifo cha Kanumba kimeathiri vipi maisha yako ya kisanii?
Pinkieto: Kanumba
alikuwa mtu muhimu sana kwangu, kufariki kwake nilihisi kama ndoto zangu
zimezimika ghafla. Namshukuru Mungu alinipa nguvu ya kuendelea
kupambana mpaka leo.
Ijumaa: Ulipotoka kwa Kanumba ulienda kufanya kazi wapi?
Pinkieto: Nilienda
kufanya kazi kwa Masanja Mkandamizaji ambaye alinipa nafasi kama ileile
(usekretari). Nikafanya pale kwa muda kisha baadaye nikaamua kujiajiri.
Vicent Kigosi ‘Ray the Gratest’
Ijumaa: Umesema kwa sasa umejiajiri ni kazi gani unaifanya?
Pinkieto: Nafanya biashara, nashukuru Mungu inaniingizia kipato lakini pia na sanaa sijaacha ndiyo kwanza nimejikita zaidi.
Ijumaa: Usekretari uliusomea au marehemu Kanumba aliamua kukuweka tu ili umsaidie?
Pinkieto: Kiukweli
wakati naanza kazi sikuwa nimesomea lakini niliingia chuo nikiwa kwa
Kanumba. Chuo kilikuwa karibu na ofisini kwetu hivyo nilikuwa nikisoma
baada ya kazi.
Ijumaa: Nini unaweza kukikumbuka kwa Kanumba?
Pinkieto: Ni vingi
kiukweli kwani nilikuwa na ndoto ya kufanya naye kazi lakini kama
ujuavyo mlango mmoja ukifungwa, unafunguliwa mwingine na ndiyo maana
nilipata nafasi kwa Masanja.
Ijumaa: Je, una mchumba au umeolewa? Vipi kuhusu usumbufu wa wanaume wakware?
Pinkieto: Ninaye mpenzi si mchumba! Kuhusu usumbufu wa wanaume upo sana tu, kikubwa ni kujitambua na kujiheshimu.
Ijumaa: Unalizungumziaje tatizo la madairekta kuwataka kimapenzi wasanii kabla ya kuwapa nafasi za kuigiza? Wewe limewahi kukukumba?
Pinkieto: Suala hilo
lipo sana na mimi lilishanitokea. Nilimpa makavu yule dairekta na
nawasihi wanaofanya hivyo waache kwani mbali na kujidhalilisha pia
linaua sana sanaa.
Ijumaa: Kipi kinaku-kwaza kwenye tasnia ya filamu kwa sasa?
Pinkieto: Wasanii hatu-pendani, tuna-chukiana kitu ambacho si kizuri, tasnia yetu hatuwezi kuijenga kwa chuki.
Ijumaa: Je, unalizungumziaje soko la sanaa kwa sasa maana linaonekana kama limeshuka?
Pinkieto: Soko la sanaa kwa sasa halina ushindani kama zamani. Enzi zile bwana, hapa Kanumba, pale JB kule Ray, ilikuwa full ushindani.
Ijumaa: Unapendelea kufanya nini ukiwa na mpenzi wako?
Pinkieto: Napenda tuangalie muvi, tuogelee pamoja au tukae tu ndani tupige stori.
Note: Only a member of this blog may post a comment.