Sunday, March 6, 2016

Anonymous

TRA Yamkalia Kooni Mbunge wa CCM, Profesa Anna TIBAIJUKA


TRA imemtaka Profesa Tibaijuka kulipa zaidi ya Sh. milioni 500 kutoka katika mgawo wa Sh. 1.62 bilioni zinazohusishwa na fedha zilizochotwa katika Akaunti ya Tegeta Escrow
Amepinga madai hayo na kukata rufaa kupinga TRA kumtaka alipe kiasi hicho cha kodi, adai hajawahi kupokea fedha hizo kutoka kwa James Rugemalira.


Inadaiwa kuwa Profesa Tibaijuka, ambaye aliondolewa katika wadhifa wake wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutokana na sakata hilo, aliwekewa fedha hizo kwenye akaunti yake na James Rugemalira, Mkurugenzi wa VIP Engineering & Marketing Limited iliyokuwa kati ya wanahisa wa IPTL.
Kutokana na mgawo huo, Desemba 31, 2015, TRA ilimtaka alipe kodi hiyo, baada ya kushindwa kufanya marejesho kutokana na mgawo huo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.