Ray c akiwa hoi na kinachodaiwa kuwa ni utumiaji wa madawa ya kulevya.
Stori: Musa Mateja, Wikienda
DAR ES SALAAM: LICHA ya kutumia nguvu nyingi kukanusha habari zinazochapishwa na Magazeti Pendwa ya Global Publishers kuwa, amerejea kwenye matumizi ya madawa ya kulevya ‘unga’, hatimaye staa wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amenaswa ‘laivu’ akiwa ‘ameangusha gari’ kando ya barabara, habari ndiyo hiyo!

Ray C ambaye kila anapoandikwa na Magazeti ya Global kuhusu kurejea
kwenye unga, amekuwa akimtupia shutuma Mkurugenzi wa Global, Eric
Shigongo kwamba anamchafua, alinaswa na mapaparazi wetu hivi karibuni
maeneo ya Mwananyamala Magengeni, Dar akiwa amezima yeye na mwanaume
aliyekuwa naye hali iliyompa urahisi paparazi wetu kuwafotoa picha za
kutosha.
ISHU ILIANZA JANUARI
Januari mwaka huu, gazeti hili liliripoti habari iliyokuwa na kichwa; CHIMBO LA UNGA LA RAY C LAGUNDULIKA.
Baada ya habari hiyo kutoka, Ray C aliikanusha kupitia ukurasa wake wa Instagram akisema:
“Seriously kwa kweli huwa naumia sanasana kuona binadamu mwenzangu anadiriki kuniharibia jina langu ili yeye apate kula! Hamjui mnaniathiri kiasi gani na hizi habari zenu! Hiyo habari yaani ni ujingaujinga tu umeunganishwa na picha yangu bila hata uoga mmeichukua kutoka kwenye page yangu ya Insta. Mnazitumia kunichafulia jina langu tena wakati ndiyo kwanza nahangaika kurudi kwenye kazi yangu.”

TV ANDAGRAUNDI IKAMSAPOTI
Kama hiyo haitoshi, kituo kimoja cha runinga cha muda mrefu nchini lakini bado kiko ‘andagraundi’ kilimpa nafasi Ray C akanushe habari ya Ijumaa Wikienda pasipo kujua gazeti hili lilijiridhisha kabla ya kuandika habari hiyo.

SHIGONGO ATAKA UKWELI
Baada ya Ray C kuyaponda Magazeti ya Global kwenye runinga kwa kudai
yanamchafua, Shigongo alimuagiza Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa,
Oscar Ndauka kupanga makachero kutokea kwenye kikosi maalum cha
Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ili kufuatilia nyendo za msanii huyo kama
kweli anaonewa au la na kutaka matokeo yaliyo kamili!
Timu ya OFM ilipangwa kwa zamu kumfuatilia Ray C kwa saa ishirini na nne ili kujiridhisha juu ya malalamiko yake, hasa kwamba Global inaungaunga picha za zamani ili kupata habari kama alivyosema kwenye Instagram yake.
Tangu Januari hiyo, timu ya OFM ilianza kuwa sambamba na Ray C huku
makachero wengine wakiwasaka watu wake wa karibu ili kusikia chochote
kutoka kwao.
Note: Only a member of this blog may post a comment.