Kwa mara ya kwanza klabu ya KRC Genk ya
Ubelgiji ambayo inaongozwa na kocha lakini inachezewa na nahodha wa timu
ya taifa ya Tanzania Mbwana Ally Samatta, imempa nafasi ya kuanza
katika mchezo wa leo dhidi ya klabu ya KV Oastende.
Samatta amepata nafasi hiyo ya kuanza
mchezo wa leo March 13, ikiwa ni zaidi ya mechi nne amekuwa akiichezea
timu hiyo akitokea benchi. Baada ya Samatta kuanza first eleven,
alipachika goli la kwanza kwa timu yake dakika ya 25 ya mchezo, lakini
hilo pia ni goli lake la pili toka ajiunge na KRC Genk.
Goli la Samatta lilifuatiwa na neema kwa
KRC Genk, kuibuka na ushidi wa goli 4-1, magoli ya KRC Genk yalifungwa
na Mbwana Samatta dakika ya 25, Balley dakika ya 39, Pozuelo dakika ya
81 na Camargo dakika ya 88, wakati goli la kufutia machozi kwa KV
Oostende lilifungwa na Siani dakika ya 90.
Note: Only a member of this blog may post a comment.