Thursday, March 10, 2016

Anonymous

NAY wa Mitego Afunguka Sababu za Kutowataja DIAMOND na ALIKIBA Kwenye Ngoma Zake

‘’Sikutaka kulizungumzia hili lakini nilijua watu watajaji,hata kwenye ‘comments’ watu wengi wanasema kwanini sijamuimba rafiki yangu Diamond na ana skendo nyingi’’ Alisema Nay Wa Mitego.

‘’Unajua sitaki kufanya kitu ambacho kila mtu tayari anacho kichwani mwake ili ni jawabu tosha kwa watu ambao wanajaji hilo kila mtu angekuwa anategemea ningemdisi Ali Kiba au Diamond sikutaka na kama ningeamua kuwazungumzia hawa watu mimi nazungumzia vitu ambacho kila mtu angekuwa nacho kwenye kichwa chake kama aliwahi kukifikiria lakini hawezi kuhisi kama kuna mtu kukizungumzia ina maana kila mtu alikuwa akitegemea anataka kuona nimemzungumzia Diamond au Ali Kiba’’Aliongeza Nay Wa Mitego.


’Sijafanya hivyo kwa makusudi tu ijapokuwa kuna vitu vya kuzungumza juu yao lakini kulikuwa hakuna umuhimu sana kuna watu walikuwa na vitu muhimu sana ndio maana hii imeenda kiasi hicho’’Alimaliza Nay

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.