Stori: MAYASA MARIWATA NA HAMIDA HASSAN
MUUZA nyago anayefanya poa
Bongo, Asha Salum ‘Kidoa’ anadaiwa kumkimbia mama yake aliyekuwa akiishi
naye maeneo ya Kinondoni na kwenda kuishi na mwanaume (jina
linahifadhiwa kwa sasa) maeneo ya Tabata jijini Dar.
Chanzo makini kimetutonya kuwa, tangu
mwanadada huyo awe staa, amekuwa si mtu wa kukaa na mama yake badala
yake amekuwa kiruka njia, usiku anaenda klabu, mara kasafiri kwenda nje
lakini siku zote analala na kuamkia kwa mwanaume huyo.
“Unajua Kidoa siku hizi kamkimbia kabisa
mama yake, muda mwingi yupo kule Tabata kwa bwana wake wakati bi mkubwa
alishazoea kuishi naye,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kuzipata nyeti hizo, Ijumaa lilimtafuta Kidoa ambapo alikiri kuwepo Tabata kwa ‘mtu’ wake akieleza kuwa, bi mkubwa huwa anakwenda kumuona mara mojamoja.
Note: Only a member of this blog may post a comment.