Tuesday, March 8, 2016

Anonymous

Mbunge KUBENEA Amkana DC Paul MAKONDA Kortini


Saed Kubenea, Mbunge wa jimbo la Ubungo (Chadema) (wakwanza), Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinodoni (wapili)
SAED Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Ubungo pia Mkurugenzi wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers amekana kumtusi Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, anaandika Faki Sosi.

Kubenea amekana kumtukana Makonda leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Slaam wakati akitoa ushahidi wa kesi inayomkabili kufanya hivyo iliyofunguliwatarehe 15 Desemba mwaka jana.

Kwenye kesi hiyo, Kubenea alifungiliwa madai matatu ambayo ni lugha ya matusi, kumwita Makonda mpumbavu, mjinga pamoja na cheo cha kupewa.

Katika kesi hiyo iliyopo mbele ya Hakimu Thomas Simba ambayo Kubenea alionekana kuwa na kesi ya kujibu, imeanza kusikilizwa leo baada ya mbunge huyo kuanza kutoa ushahidi wake.

Kubenea ndiye shahidi namba moja kwenye kesi hiyo ambapo ameieleza mahakama kwamba, katika vuta nikuvute iliyotokea tarehe 14 Desemba mwaka jana kwenye Kiwanda cha nguo cha TOOKU kilichopo Ubungo, jijini Dar es Salaam hakumtukana Makonda na kwamba, hatua ya kumkatalia kuzungumza na wananchi si kitendo cha kiungwana.

Kesi hiyo inaendelea kusakilizwa.
Viongozi hao wawili Desemba mwaka jana waligombana kwenye kiwanda hicho ambapo Kubenea alikamatwa na polisi kwenye eneo hilo kwa amri Makonda .

Tukio lililohusisha kukamatwa kwa Kubenea lilikuwa ni mgomo wa wafanyakazi zaidi ya 1800 wa kiwanda hicho ambao walimpigia mbunge wao aende kutatua mgogoro huo ambapo Kubenea alifika katika eneo hilo saa 6 mchana na kukutana na wafanyakazi kusikiliza kero zao za muda mrefu.

Kisha aliamua kuondoka na viongozi wa wafanyakazi hao na kufanya kikao na menejimenti ya kiwanda hicho kuanzia saa 7 hadi saa 9.

Ilipofika saa 10:30 Makonda alifika na kupata taarifa kwa muafaka uliofikiwa kati ya Kubenea, menejimenti na viongozi wa wafanyakazi.

Alitoa amri wafanyakazi wakusanyike, akaawaambia kesho atafika huko na Waziri wa Viwanda na Biashara, Waziri wa Kazi na Ajira, na Waziri wa Afya Wanawake, Jinsia na Watoto.

Baada ya kutoa maagizo hayo, Makonda alimzuia Kubenea kuhutubia na kuaga wananchi aliokuwa nao tangu mchana, kutokana na hali hiyo (Kubenea) alisema ni vema aseme neno, ndipo mvutano ulipoanza.

Makonda alimuru mkutano ufungwe lakini wafanyakazi hawakutawanyika eneo hilo, alipoona hivyo aliamrisha Polisi wamkamate Kubenea ambapo sintofahamu iliongezeka.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.