GLADNESS MALLYA Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: Haya ni mauzauza jamani!
Wakazi wa Mtaa wa Kiyombo Shule, Nyantira Kata ya Kitunda jijini Dar
wamejikuta katika wakati mgumu kutokana na eneo hilo kutawaliwa na
mauzauza ya kurushiwa mawe na kupigwa fimbo na watu wasioonekana hali
inayowafanya washindwe kulala.
Akisimulia kwa masikitiko makubwa, mkazi mmoja ambaye ni mwathirika wa tukio hilo aliyejitambulisha kwa jina la mama Kasim alisema mawe hayo huanza kurushwa kwenye mabati juu ya nyumba kuanzia saa tatu usiku lakini wakitoka nje hawamuoni anayerusha na mawe pia.
Akisimulia kwa masikitiko makubwa, mkazi mmoja ambaye ni mwathirika wa tukio hilo aliyejitambulisha kwa jina la mama Kasim alisema mawe hayo huanza kurushwa kwenye mabati juu ya nyumba kuanzia saa tatu usiku lakini wakitoka nje hawamuoni anayerusha na mawe pia.
Viongozi wa Serikali ya Mtaa huo wakiongoza kikao.
“Ukweli tunateseka. Hatujui ni kitu gani
kwani kuna kipindi yakianza kurushwa hivyo wote hapa nyumbani kwangu
tunaugua miguu na kushindwa kutembea. Hapa mtaani kila mmoja na majanga
yake, kuna wengine wanachapwa fimbo lakini wanaowachapa hawaonekani.
Wakiamka asubuhi wanakuta wana alama za fimbo huku wamevimba.
“Wachungaji waliwahi kuja kuombea hapa
kwenye nyumba ya jirani lakini walitoka nduki na kuacha kila kitu baada
ya kurushiwa mawe na mrushaji haonekani,” alisema mama Kasim.
Kutokana na mauzauza hayo, mwenyekiti wa
eneo hilo, Issa Chilemba wiki iliyopita aliitisha mkutano wa hadhara
ambapo wakazi walijianika wanavyoteseka kwa kurushiwa mawe usiku na
kushindwa kulala huku wengine wakieleza kuwa wakiamka asubuhi hujikuta
wamechanjwa mwili mzima bila kujua ni nani anayewachanja.
Kikao kikiendelea.
Pamoja na kurushiwa mawe na kuchanjwa
wapo wengine walioeleza kuwa, walivuta umeme kwenye nyumba zao lakini
uliwaka kwa siku moja na kuzima na walipoita mafundi hawakuona tatizo
zaidi ya kugundua kwamba ni mambo ya kishirikina.
Katika mkutano huo, wananchi na
mwenyekiti wao walikubaliana kuunda kamati ambayo itashughulikia suala
hilo kwa kuchunguza wachawi wanaofanya mauzauza hayo, pia kuendelea
kufunga na kumuomba Mungu kila mmoja kwa imani yake.
Moja ya nyumba ya familia hizo.
“Kiukweli hili jambo ni la aibu na
limenikera sana. Tunaweza kuleta mtaalam ‘sangoma’ hapa akawaumbua watu
na heshima zao, hivyo nawaomba wanaofanya hivyo waache. Au kama kuna mtu
anayedhaniwa kufanya hivyo naombeni mnipe jina lake kwa siri.
“Kupitia kamati hii maalum tunayounda
ikipata majibu tutafanya maamuzi magumu ambapo atakayegundulika kwamba
ndiye anayefanya mauzauza haya atahamishwa eneo hili,” alisema
mwenyekiti huyo.
Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo, mwaka
2013 kulikuwa na tatizo kama hilo lakini waligundua kwamba ni kijana
mdogo aliyekuwa akitumiwa kichawi na bibi yake ambapo walimrudisha kwao
mkoani Njombe lakini Februari, mwaka huu mauzauza hayo yalianza tena.

Note: Only a member of this blog may post a comment.