Wednesday, March 9, 2016

Anonymous

Maswali 5 SEFUE Kung’olewa Ikulu!

 Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Balozi Ombeni Sifue
Na Elvan Stambuli, RISASI mchanganyiko
GUMZO kubwa sehemu mbalimbali nchini hivi sasa ni kuhusu kung’olewa Ikulu bila kutajwa sababu kwa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sifue hali inayozua maswali matano yanayokosa majibu.
Balozi Sefue aliyekuwa kiungo muhimu wa serikali, aliondolewa katika wadhifa huo na Rais John Pombe Peter Magufuli Jumapili iliyopita na nafasi yake kuchukuliwa na Injinia John Kijazi, aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini India.

Wachunguzi wa mambo ya kisiasa wanasema Katibu Mkuu Kiongozi ni katibu wa baraza la mawaziri na walio juu yake ni rais ambaye ni mwenyekiti wa baraza hilo, makamu wa rais na waziri mkuu huku mawaziri wakiwa ni wajumbe, hali inayozidisha maswali mengi.

Kung’olewa kwake kunafanya wachunguzi hao wa mambo ya kisiasa kujiuliza kwa nini awe ameteuliwa Desemba na ndani ya miezi mitatu ang’olewe?
Wapo wanaojiuliza kuwa huenda kuondolewa kwake kumetokana na baadhi ya vyombo vya habari vilivyomtaja katika tuhuma mbalimbali mbaya?
Baadhi ya wasomi ambao hawakutaka kutajwa majina yao gazetini, wanahoji kung’olewa kwake kunahusiana na utawala wa Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, ambao umedhihirika sasa kuwa watendaji wake walikuwa na ‘figisufigisu’ nyingi?
Wengine wanasema huenda kuondolewa kwake kunatokana na ukweli kwamba Sefue siyo kizazi cha utawala wa Magufuli? Inasemekana kasi ya utendaji kazi wa serikali iliyopo madarakani hivi sasa inahitaji watu wasio na aibu katika utekelezaji wa majukumu yake.

Lakini pia wapo wanaohoji huenda rais Magufuli alimuacha ili ampe kwanza uzoefu wa Ikulu?
Hata hivyo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar, Dk Haji Semboja amesema aonavyo yeye, kuondolewa kwa Sefue hakuna uhusiano wowote na utumbuaji wa majipu bali ni utaratibu wa kawaida wa watawala pindi wanapoingia madarakani.

“Kikwete alipoingia madarakani alimteua Philemon Luhanjo kuchukua nafasi ya Marten Lumbanga aliyemkuta hivyo yaliyotokea ni kawaida,” alisema Dk. Semboja.
Injinia Kijazi aliwahi kuwa katibu mkuu wa Wiraza ya Ujenzi na Miundombinu kipindi ambacho Rais Magufuli alikuwa waziri wa wizara hiyo mwaka 2000 na 2005.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.