Fatuma Makame ‘Joanitha
Na Hamida Hassan
Staa wa Filamu Bongo, Fatuma Makame ‘Joanitha’ na Video Queen Gift
Stanford ‘Gigy Money’ wanatarajia kuchuana kwenye filamu watakayocheza
pamoja hivi karibuni baada ya Gigy kuchukuliwa na Kampuni ya Hamadombe
kwa majaribio.
Akizungumza na Ijumaa, Joanitha ambaye ni bosi wa kampuni hiyo
alisema wamebaini Gigy anao uwezo mzuri wa kuigiza lakini hajapewa
nafasi hivyo wameona wakati anaendelea na U-Video Queen wake pia acheze
filamu.
Gift Stanford ‘Gigy Money’
“Unajua kwa sasa tumeamua kuwachukua wasanii kama ‘brand’ ili
kushindana na makampuni mengine kwenye uigizaji hivyo tumemchukua Gigy
Money na Tiko Hassan ambao wataingia kambini muda si mrefu,” alisema
Joanitha.

Note: Only a member of this blog may post a comment.