Saturday, March 19, 2016

Anonymous

Maalim Hassan Autabiria Uchaguzi wa Zanzibar


shekhe yahya hussen
Mtabiri maarufu nchini, Maalim Hassan Yahya Hussein
Elvan Stambuli, Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: Mtabiri maarufu nchini, Maalim Hassan Yahya Hussein ameutabiria uchaguzi wa marudio wa Zanzibar unaotarajia kufanyika kesho visiwani humo.
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum ofisini kwake Dar juzi, Maalim Hassan alisema uchaguzi huo utafanyika kwa amani na wala hakutakuwa na fujo.
“Uchaguzi utapita salama na mshindi atapatikana, kinyota inaonesha hakutakuwa na purukushani zitakazotokea wakati wa uchaguzi huo,” alisema.

Aliongeza kuwa, wananchi hawapaswi kuwa na hofu kwani hakuna ukiukwaji wa taratibu na uvunjifu wa amani utakaofanyika siku hiyo ya uchaguzi.

Hivi karibuni kumekuwa na hofu visiwani humo kutokana na matukio yanayohusishwa na siasa ambapo nyumba kadhaa zilichomwa moto kisiwani Pemba na nyumba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame ililipuliwa na kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu na watu wasiojulikana saa 5.00 usiku huko Kijichi, nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Uchaguzi wa Zanzibar unatarajiwa kurudiwa kesho baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana kufutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salum Jecha kwa madai kuwa ulikuwa na kasoro nyingi

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.