Tuesday, March 8, 2016

Anonymous

Luis SUAREZ Karudi LIVERPOOL Leo!

Mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay ambaye anaichezea klabu ya FC Barcelona ya Hispania Luis Suarez, March 8 ameingia kwenye headlines baada ya mtandao wa sokka.com kuandika na kutoa picha za staa huyo akiwa Liverpool.
Suarez amerejea leo Liverpool kuwatembelea na kuwasalimia rafiki zake katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo Melwood, Suarez amecheza ndani ya klabu hiyo kwa zaidi ya miaka miwili, kabla ya mwaka 2014 kuamua kujiunga na klabu ya FC Barcelona ambayo anaichezea hadi sasa.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri, Luis Suarez aliwahi kuichezea klabu ya Liverpool kuanzia mwaka 2011 baada ya kujiunga na klabu hiyo akitokea klabu ya Ajax ya Uholanzi ambayo alidumu nayo kwa miaka minne, lakini mwaka 2014 ndio akajiunga na FC Barcelona.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.