Monday, March 14, 2016

Anonymous

Kiiza: SIMBA SC Msimuachie KESSY Aende YANGA SC


Hassan-‘-Kessy’-Ramadhani2
Beki Hassan Kessy.
Wilbert Molandi,Dar es Salaam
MSHAMBULIAJI wa kutegemewa wa Simba, Mganda, Hamis Kiiza, ametoa ushauri wa bure kwa viongozi wake. Amewaambia kuwa kama kuna kosa kubwa watakalolifanya ambalo litawafanya wajutie, basi ni kumuacha beki Hassan Kessy aende Yanga.
Kiiza ambaye amewahi kuichezea Yanga, ametoa kauli hiyo baada ya kupata taarifa kuwa Kessy anawaniwa na klabu hiyo.
HAMISI-KIIZA.jpgMshambuliaji wa kutegemewa wa Simba, Mganda, Hamis Kiiza.
Kessy inadaiwa hivi karibuni aligoma kusaini mkataba mpya Msimbazi, akidai dau nono la shilingi milioni 60.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Kiiza alisema beki huyo ndiye aliyefanikisha kwa kiwango kikubwa idadi ya mabao 18 aliyofunga msimu huu wa Ligi Kuu Bara.
“Kessy ni mpishi mzuri wa mabao ambaye amehusika kwa kiwango kikubwa kunitengenezea mabao mengi tofauti na wachezaji wengine kiukweli.

“Wapo wachezaji wengine walionitengenezea nafasi za kufunga, lakini kwake Kessy ni nyingi sana, amenitengenezea kwa njia ya krosi na kona anazopiga.
“Hivyo, viongozi ni vyema wakapambana vya kutosha kuhakikisha wanambakiza Kessy ili asiende huko Yanga wanaotaka kumsajili,” alisema Kiiza.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.