Monday, March 7, 2016

Anonymous

Kama Ulikamatwa na Traffic Dar Kati ya Feb 28 Mpaka March 7, Faini Yako Imejazia Hizi Milioni!

Kikosi cha Usalama Barabarani kanda maalum ya Dar es salaam kimetangaza kukusanya kiasi cha shilingi Milioni 365 kutokana na ukamataji wa makosa ya usalama Barabarani kwa kipindi cha kuanzia February 28 2016 hadi March 07 2016.
Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Simon Sirro amesema…>>>‘Hatusemi kwamba lengo letu kukusanya mapato mengi kwamba ni sifa sana kwetu, hapana tunafanya hivyo ili watu wafuate sheria na hatufanyi hivyo ili kuwakomoa watu, kikubwa kufuata tu sheria‘:-Simon Sirro
HIZO MILIONI 365 ZIMETOKANA NA HII LIST HAPA CHINI
  1. IDADI YA MAGARI YALIYOKAMATWA    –8,647
  2. IDADI YA PIKIPIKI ZILIZOKAMATWA     –3,851
  3. DALADALA ZILIZOKAMATWA                 –5,130
  4. MAGARI MENGINE (BINAFSI NA MALORI)    –3,517
  5. JUMLA YA MAKOSA YALIYOKAMATWA     –11,950

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.