Monday, March 7, 2016

Anonymous

Jackson MAYANJA: Sipo Tayari Kupangiwa Kikosi na Kiongozi Yeyote wa Klabu SIMBA SC

Kocha wa klabu Simba, Jackson Mayanja, amesema kuwa yupo tayari kufukuzwa kazi Simba endapo atapangiwa kikosi na kiongozi yeyote wa klabu hiyo.
picmayanja-559x520
Kauli hiyo ya Mayanja imekuja siku chache baada ya Kamati ya Utendaji ya timu hiyo kumsimamisha nahodha wake msaidizi, Hassan Isihaka kwa muda usiojulikana kwa kuonesha kitendo cha utovu wa nidhamu kwa kocha wake.
“Kumiliki mchezaji ni jambo ambalo linatumika sehemu nyingi si hapa Tanzania, kwani hata Ulaya wanafanya hivyo lakini mchezaji atacheza kulingana na mipango ya kocha na si mtu tofauti kupanga timu ya kucheza.

“Sikuwahi kupangiwa na hakuna wa kunipangia mchezaji wa kucheza kwenye klabu hii, mimi ni kocha ninayefuata misingi ya taaluma yangu hivyo sitaweza kuogopa kusema ukweli, ndio maana nimelizungumza hili bila hofu ili kila mtu afahamu wajibu wake,” alisema Mayanja.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.