Wengi
wamefurahia ushindi wa Waigizaji wa Tanzania Lulu pamoja na Richie
kwenye tuzo za Africa Magic Viewer’s Choice Awards 2016 na sasa
tumeendelea kushuhudia comments na post mbalimbali kwenye mitandao ya
kijamii baada ya ushindi huo ambapo uhuru ambao kila mmoja anao kuandika
chochote kwenye mitandao hii unaweza kufikia kukwaza watu wengine
Lulu
ambaye alishinda tuzo ya Movie bora Afrika Mashariki kupitia movie yake
ya ‘Mapenzi’ alihuzunishwa na post moja iliyoandikwa kwenye mtandao wa
Instagram ikisema >>> ‘Jamani
umbea mtamu khaaaa, yani umbea mtamu kama kuku jamani, bwana leo kuna
mtu kanifata DM kanipa Umbea na mimi sitaki kuongeza chumvi‘
‘Haya
soma mwenyewe, mambo Duller? naomba unifiche jina langu, ni kweli
kabisa Lulu anahusika na ajali iliyotokea jana watu wakafa wengi, mimi
nipo Nigeria, alimuomba rafiki yangu Mnigeria ampeleke kwa mganga mkubwa
hata wa kitoa kafara yeye atafanya, kwa mganga akaambiwa aongee yote
chini ya mti na dawa akapewa ya kutupa njia panda yoyote usiku wa manane‘
Ajali iliyotokea Dar es salaam
‘Haya
nimeambiwa na Mnigeria ambaye kampeleka ambaye ni Bwanaangu, sasa jana
baada ya kumuonyesha picha ya ajali iliyotokea akasema sawa kabisa huyo
ni Lulu sababu aliambiwa asipitishe siku mbili majini hayatakaa Tanzania
zaidi ya siku mbili
Baada ya Lulu kuiona hii post aliichukua kama ilivyo na kuiweka kwenye page yake ya Instagram na kuandika yafuatayo… ‘Jamani
mpaka sasa hivi mshaongea vitu vingi sana na nimekaa kimya, okay kwa
hili siwezi kujua ni watu kiasi gani wataamini na wengine hawataamini,
kilichonifanya nipate tuzo au mafanikio ni Mungu, juhudi zangu pamoja na
watu walionipigia kura‘
‘Sijawahi
na wala sina fikra za kutumia nguvu yoyote ya ziada kupata mafanikio,
kama mnahisi maneno na uongo vinaweza kunirudisha nyuma kwa hali yoyote
nawaombeeni muishi maisha mengi muone Mungu anavyozidi kuniinua, wewe
uliyepost na huyo aliyekutumia msg sibishani na nyie ila imani yangu
ntaongea na Mungu wangu tu, mtajutia mlichokifanya hata kama ikiwa baada
ya miaka 50 mana najua Mungu anajibu kwa wakati‘
Note: Only a member of this blog may post a comment.