Tuesday, March 8, 2016

Anonymous

HABARI NJEMA: Mwanafunzi Aliyeongoza Kitaifa Matokeo Kidato Cha Nne Apata Shavu Nene Benki ya CRDB

Benki ya CRDB imemfungulia Akaunti ya Scholarship na kumwekea sh. Milioni 5 mwanafunzi aliyefanya vizuri katika mtihani wa kumaliza kidato cha nne mwaka 2015, Butogwa Shija na kumwahidi ajira pindi amalizapo masomo.

Hafla hiyo ilifanyika jana jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani leo, ambapo Butogwa alipewa zawadi ili kuwahamasisha watoto wa kike kwamba wanaweza.

Pia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ilimuongezea mwanafunzi huyo kiasi cha shilingi 500,000 lengo likiwa ni kuwahamasisha watoto wa kike ili kuleta haki sawa kwa wote.

Naye Butogwa aliahidi kutumia fursa hiyo vizuri kwa kusoma kwa bidii bila kubweteka na kuwataka wanafunzi wengine kuweka bidii kwenye masomo yao.

Katika hatua nyingine, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Esther Kitoka alisema wametoa sh. milioni 20 zitakazosaidia katika ujenzi wa mabweni kwa watoto wa kike ili kuongeza kasi ya ufaulu kwa wanafunzi

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.