Tuesday, February 23, 2016

Anonymous

VIDEO: Zaidi ya Trilioni 1 Zilivyokusanywa na Kugawanywa Ndani ya Mwezi Mmoja Katika Serikali ya Rais MAGUFULI

Serikali imefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi trilioni moja kwa mwezi huu tofauti na zilizokuwa zikukusanya hapo awali za bilioni 850 kwa kipindi cha mwezi mmoja na kuzielekeza fedha hizo kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo. 

Takwimu hizo zimetolewa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango  Dkt. Servacius Likwelile wakati akitoa taarifa ya hali ya mapato kwa kipindi cha mwezi Februari mwaka huu. 

Likwelile amesema ‘kati ya fedha hizo ,sekta ya elimu imepewa shilingi bilioni 18.7  kwa ajili ya utekelezaji wa utoaji wa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za awali hadi kidato cha Nne ambapo fedha hizo ni kwa ajili ya malipo ya ada,chakula pamoja na ruzuku‘. 

Mkoa wa Dar es salaam  imeongezewa shilingi bilioni 2 ili kupanua uwezo wa udahili kama Rais alivyoahidi katika mkutano wake na Wazee wa Mkoa huo na kati ya fedha hizo  wakufunzi wamepatiwa shilingi milioni 431.6 walimu walio masomoni wametengewa  shilingi milioni 249.2 kwa ajili ya vifaa vya kufundishia, posho na nauli 

fedha nyingine kati ya hizo kiasi cha shilingi bilioni 573.7 zimetolewa kwa ajili ya  mishahara ya watumishi wa Umma  , ulipaji wa deni la taifa kwa mwezi huu zimetolewa shilingi bilioni 842.1 na Mifuko ya hifadhi za Jamii zimetolewa shilingi bilioni 81.13
Unaweza kumtazama hapa Katibu Mkuu Dkt. Servacius Likwelile

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.