Nguli wa Hip Hop nchini, Joseph Haule ‘Professor Jay’.
Hans Mloli
NGULI wa Hip Hop nchini, Joseph Haule ‘Professor Jay’
ambaye kwa sasa ni mbunge wa jimbo la Mikumi, Morogoro amefunguka mengi
kuhusiana na maisha yake mapya ya ubunge kwa sasa lakini pia akagusia
jinsi gani asivyopenda kuitwa mheshimiwa na muda gani ataendelea na kazi
yake ya muziki.Aidha, pia ameelezea fursa na nafasi nyingi anazozipata za kukamilisha mambo yake mapema baada ya kuwa na wadhifa huo kwa kuwa ana uwezo wa kuonana na watu wa ngazi za juu muda wowote na mambo yanakaa sawa ambavyo ni tofauti na ilivyokuwa kitambo.
“Lakini katika vitu ambavyo sivipendi katika ubunge ni kuitwa mheshimiwa, napenda kuitwa mtumishi. Neno mheshimiwa linatenganisha ukaribu wangu na jamii, wanaweza kuona kama mtu nisiyeguswa badala yake mimi ni mtumishi wao, wanapaswa kuniagiza na kuwatumikia katika mahitaji yao,” alisema Professor Jay.

Note: Only a member of this blog may post a comment.