Mama Salma Kikwete (kulia) akimfariji
mama mzazi wa Banza Stone, Bi. Khadija Masanja (kushoto) enzi za uhai
wake. (Picha na Maktaba yetu)
PIGO limeikumba familia ya mwanamuziki nyota wa muziki wa dansi,
marehemu Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ marehemu Banza Stone baada ya
kuondokewa na watu wawili wazito leo hii ambao ni mama mzazi na mtoto wa
dada yake.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa aliyeanza kufariki dunia ni mtoto wa
dada yake Banza Stone aitwaye Sozi Masanja ambaye alikuwa akiugua kwa
siku kadhaa ambaye kafariki saa mbili asubuhi.
Masaa mawili baadaye mama mzazi wa Banza Stone, Bi. Khadija Masanja
naye akafariki dunia kwa kile kinachodhaniwa kuwa ni kutokana na
mshituko wa kufiwa na binti yake.
Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi. AMEN.

Note: Only a member of this blog may post a comment.