Nay wa Mitego
Na Chande Abdallah na Mtandao
WAKATI msanii Nay wa Mitego akijijengea jina kwa nyimbo zenye maudhui
ya kuwachana au kuwatusi mastaa wenzake huku Wimbo wa Shika Adabu Yako
ukipitiliza kiasi cha kufungiwa na BASATA, soma kidogo kuhusu mkali wa
Rap kutoka Marekani, Marshall Mathers ‘Eminem’; Nay wa Mitego hamfikii
hata robo kwa mitusi.
Eminem
Kwa mujibu wa mitandao ya kijamii nchini
Marekani imeorodhesha watu zaidi ya mia moja waliotukanwa na Eminem
kupita nyimbo zake huku kwenye idadi hiyo wakiwemo marais kama vile
George Bush, Bill Clinton na makamu wake Chris Cheney.
Kama hiyo haitoshi Eminem ameshawahi kuwatukana watu muhimu katika
maisha yake wakiwemo, mama yake mzazi, Debbie Mathers kwenye traki zake
kama vile; Clean Out My Closet na My Mom huku akimuunganisha mke wake wa
zamani, Kim kwenye Wimbo wa Kill You.
Baadhi ya mastaa aliowahi kuwatukana kwenye traki zake tofauti ni
kama vile: Christina Aguilera, Britney Spears, Will Smith, Jessica
Simpson, Rihanna, Kim Kardashian, Michael Jackson, Jarule, Dr Dre,
Milley Cyrus, Mariah Carey, P Diddy na wengine kibao.

Note: Only a member of this blog may post a comment.