Mariam Juma aliyepatikana akiwa mtupu katika shimo lenye urefu wa futi kumi, nyumbani kwa tajiri.
Stori: Makongoro Oging’, Uwazi
DAR ES SALAAM: Mariam Juma (25), maarufu kwa jina la Upa ambaye
alidhaniwa na wananchi kuwa ni msukule baada ya kupatikana akiwa mtupu
katika shimo lenye urefu wa futi kumi, nyumbani kwa tajiri aliyejulikana
kwa jina moja la Mtei Januari 19, mwaka huu, Kibamba, Wilaya ya
Kinondoni jijini Dar, anaendelea vizuri kiafya katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili tofauti na alivyofikishwa hapo kwa mara ya kwanza.
‘Msukule’ wa tajiri aendelea vizuriAidha, Mohamed aliendelea kusema kwamba Upa yupo Muhimbili katika kitengo cha watu wenye matatizo ya akili anakofanyiwa uchunguzi na matibabu na kwamba amekuwa akienda kumjulia hali na kumpelekea chakula ambapo hata yeye amekuwa akijisikia vizuri anapomuona mumewe, jambo ambalo linamfanya wale naye pamoja, kuzungumza kisha kuagana.
“Kwa mara ya kwanza alipopatikana katika shimo nyumbani kwa tajiri na kutoweka akiwa mikononi mwa polisi kisha kupatikana tena kwenye bonde la Mto Msimbazi, kuna tofauti kubwa. Namuombea kwa Mungu apone haraka arudi nyumbani kwani watoto wamekuwa wakimlilia,” alisema Mohamed.
Upa aliaga nyumbani kwa dada yake mkubwa anayeishi Tabata Matumbi, Dar mwanzoni mwa mwezi Januari, mwaka huu akidai anakwenda kuwanunulia nguo wanaye katika Soko la Buguruni lakini hakurudi nyumbani ambapo baadaye alipatikana katika shimo, nyumbani kwa Mtei.

Note: Only a member of this blog may post a comment.