Sunday, February 21, 2016

Anonymous

Mbwana SAMATTA Achanja Mbuga KRC Genk, Tazama VIDEO Yake ya Jana Jumamosi Uwanjani Hapa

Mshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta February 20 2016 ametimiza jumla ya dakika 60 za kuitumikia klabu yake ya sasa ya KRC Genk ya Ubelgiji, ambayo alijiunga nayo mapema mwezi January mwaka huu akitokea TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. 

Samatta ambaye amekuwa akiingia akitokea benchi katika mechi zake zote tatu alizocheza akiitumikia timu hiyo, ametimiza jumla ya dakika 60 za kuitumikia Genk, baada ya kupata nafasi ya kucheza kwa dakika 30 akitokea benchi katika mechi dhidi ya Lokeren, baada ya dakika ya 60 kuingia kuchukua nafasi ya Nikolaos Karelis. Mechi ya kwanza ya Samatta kuichezea Genk alicheza kwa dakika 17 ya pili kwa dakika 13 na February 20 akacheza jumla ya dakika 30. Hii ni video ya sehemu ya mechi yao mtu wangu.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.