Kuelekea SIMBA, YANGA: Fedha za MANJI Zaivuruga SIMBA SC
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji.
Khadija Mngwai, Dar es Salaam
IKIWA imebakia siku moja mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga ifike, presha ya mchezo imekuwa kubwa ambapo inadaiwa kuwa uongozi wa Simba umesita kutoa ahadi ya fedha kwa kumhofia mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kuwa anaweza kuwapandia dau wachezaji.
Simba na Yanga zinatarajiwa kukutana kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara ambapo imeelezwa ukimya wa ahadi ya fedha unatokana na hofu hiyo.
Chanzo cha kuaminika kutoka Simba kimeeleza kuwa, mvutano mkubwa kuhusu ahadi ya fedha kwa wachezaji unatokana na hofu hiyo kwa kuwa kama wao wakitangaza kisha Manji akapanda dau kwa kuahidi kuwapa fedha nyingi wachezaji wake, basi inaweza kuwavuruga Simba.
“Viongozi wetu wanahofia hilo kwa kuwa wanajua Manji akiwapandia dau tu wao hawatakuwa na nguvu ya kupanda zaidi yake, hivyo kisaikolojia inaweza kuwavuruga wachezaji wa Simba,” alisema mtoa habari huyo.
Hakuna kiongozi wa Simba ambaye alikuwa tayari kuthibitisha juu ya hilo.
USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)
Note: Only a member of this blog may post a comment.