Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa ripoti ya mwenendo wa ugonjwa wa Kipindupindu nchini kwa mwezi wa February 2016
Akiongea na Waandishi wa Habari Dar es salaam, Naibu Waziri Dk. Hamisi Kigwangalla amesema ‘Takwimu
za wiki iliyopita zinaonyesha kuwa kuanzia tarehe 22 hadi 28 ya mwezi
Februari 2016, idadi ya wagonjwa wapya walioripotiwa ni 473, na kati yao
watu 9 walipoteza maisha.‘
‘Jumla
ya Mikoa 12 nchini iliripoti wagonjwa katika kipindi cha juma moja
lililopita ambapo Mkoa wa Mara uliripoti idadi kubwa zaidi ya wagonjwa
ambao ni 125, Iringa 64, Mwanza 59, Morogoro 44, Mbeya 29, Dar es salaam
25, Arusha 18, Kigoma 8, Rukwa 6, Simiyu 6 na Singida 2‘
‘Wizara
inaendelea kutoa rai kwa jamii, Wataalamu na viongozi katika ngazi zote
kwamba kila mmoja wetu atimize wajibu wake katika harakati za
kuudhibiti ugonjwa wa Kipindupindu‘
Note: Only a member of this blog may post a comment.